|
Karibu Halmashauri ya Manispaa ya Ilala |
|
Dira: Kuwa na Jamii yenye maisha bora ifikapo 2025
Dhima:Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ina Jukum la kufanikisha dira ya kuwa na maisha bora kwa wakazi wake kwa kuhakikisha inatoa huduma za kijamii na kiuchumi.
Mstahiki Meya Jerry Silaa
Malengo Makuu ya Halmashauri
Halmashauri imeainisha malengo makuu yafuatayo katika kufikia dhamira yake; >Huduma ya UKIMWI kuboreshwa na maambukizi mapya kupunguzwa. >Kuwa na huduma bora zilizo imarishwa >Kuongeza na kuimarisha miundombinu na huduma za kiuchumi zenye ubora >Kujenga uwezo kwa ustawi wa Jamii na Jinsia kwa ujumla >Kuimarisha na Kujiandaa na maafa yanayotokea na >Kuimarisha Utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa
Chimbuko la Halmashauri Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ilizinduliwa tarehe 1 Februari,2000 kupitia Governmnet Gazzette,Notice No.2 ya tarehe 21st Januari,2000 kufuatia kukamilika kwa marekebisho yaliounda upya Halmashauri nn(4) za Mkoa wa Dar es Salaam ambazo ni Illala,Temeke,Kinondoni na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
|
|
|
Taarifa ya Utekelezaji Ilani 2005-2010 |
|
Muhtasari wa utekelezaji miradi kwa kipindi cha mwaka 2005 hadi 2010 uko kama ifuatavyo:- · Shule za sekondari zilizokuwepo mwaka 2005 ni 25, shule zilizopo kwa mwaka 2010 ni 92. Ongezeko la shule 67 sawa na 268%. · Idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga shule za sekondari mwaka 2005 walikuwa 11,020 na mwaka 2010 ni 42,040, ongezeko la wanafunzi ni 31,020 sawa na 283%. · Idadi ya waalimu wa sekondari waliokuwepo mwaka 2005 ni 880 na mwaka 2010 ni 1700. Ongezeko la waalimu 820 sawa na 93%. · Jumla ya sekondari za serikali ni 49 na za binafsi ni 43. Hivyo jumla ya shule zote za sekondari ni 92. Idadi ya wanafunzi wa sekondari wanaosoma shule za serikali ni 42,240 na shule za binafsi ni 12,035, jumla ni wanafunzi 54,275. |
|
Read more...
|
|
|
Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania |
|
Makala maalumu ya kusheherekea miaka 50 ya Tanzania. Je wajua Chimbuko la Mkoa wa Dar Es Salaam/ Je Wajua asili ya Dar Es Salaam? Ungana na Mtaalamu wa Kiswahili na Asili ya Dar Es Salaam huyu si mwingine bali ni Shani Kitogo ..... |
|
|
|